Sunday, June 30, 2013

TUMALIZE JUMAPILI YA MWEZI NA NI DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C NA WIMBO HUU!!!


Na ujumbe wangu ni TUSAMEHEANE KATIKA BWANA...JUMAPILI NJEMA NA TUTAONANA TENA JUMAPILI IJAYO KWANI NITAPOTEA KIDOGO WIKI IANZAYO KESHO.

Saturday, June 29, 2013

KAMA WOTE TUJUAVYO AKIBA HAIOZI KWA HIYO LEO NI SIKU YA MAVUNO YA FIGIRI NA MBOGA MABOGA ..AKIBA

 Hapa Kapulya yupo kwenye bustani yake na hapo anachuma mboga ya maboga. Nimestuka ni vizuri kuweka akiba  maana msimu wa joto ni mfupi sana na muda si mrefu kutakuwa na baridi na sasa nitaweka akiba. Kuna aina mbili za kuweka akiba hizi mboga mboga na uyoga hata nyama na samaki...Kwanza unaweza kukausha kwenye jua au kuchemsha na kuhifadhi kwenye friza/jokofu na mimi nita...
chemsha  kama dakika 5-10 hivi na kuweka kwenye mifuko ya plastiki na kuweka kwenye friza  na nitakuwa nakula pale nitakapotamani..najua haiwi tamu kama kuchuma tu na kula..Hapa ni fungu moja la mboga maboga na fungu moja la figiri..mboga maboga ni mvuno wa pili na figiri mvuno wa kwanza...Kuhusu bustani....nitaendelea kuwajuza. Kwa hivyo usione unakosa  kuna akiba...karibuni na JUMAMOSI NJEMA ...TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA....KAPULYA.

TUMKARIBISHE DA´MIJA NA BLOG YAKE MPYA MIJA HAUTE COUTURE...

Na hapa ni moja ya kazi za mikono yake da´Mija ni heleni za kanga..kwa kutaka kuja zaidi kazi zake gonga HAPA. Binafsi nakukaribisha kwa mikono miwili na pia nasema HONGERA SANA.

Friday, June 28, 2013

NIWATAKIENI IJUMAA HII YA MWISHO WA MWEZI KWA MLO HUU...MAKANDE!!!

Karibuni tujumuike na mlo huu wa makande/ngánde/makandi..au sijui wewe kwa lugha yako unasemaje..Nimeona si vibaya kama Ijumaa hii ya mwisho wa mwezi huu tukimaliza kwa mlo huu mzito.Ijumaa njema na mwisho wa juma uwe mwema kwa wote.

Thursday, June 27, 2013

LEO TUANGALIA NENO WIVU....

WIVU:- Ni hali au tabia ya mtu kusononeka au kukasirika kwa muda mtu amuonapo mpenzi au rafiki yake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine. Hii ni tafsiri ya KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU.
Na hapa sasa nilikuwa namsikia marehemu mama yangu akiimba wimbo huu alikuwa mpenzi sana wa zilipendwa utadhani yeye ndio alikuwa redio:

Wivu ukizidi nyumbani mapenzi yanapungua,
Wivu usio na maana waleta hasara,
Umefanya kitu gani bibi umemkataza kufanya kazi
Ati sababu achelewa nyumbani.

Sikumbuki ni nani aliimba nilikuwa msichana mdogo kiasi kwamba hata sikujua neno wivu maana yake ni nini. Inasemekana ni muhimu kuwa na kumwenea umpendaye, Maana mapenzi bila wivu si mapenzi. Kwamba haiwezekani mtu ukae tu, vitu vinatendeka mbele ya macho yako ambavyo vyaweza kukutia mashaka na wewe ukakaa tu bila kuona wivu. Huo ni ubinadamu kwani binadamu tuna silka ya wanyama, huwa tunaweka maeneo yetu alama kama wanyama ili wasiingiliwe na wengine.Hii yote ni kuonyesha wivu.......!!!Wengine wanasema wivu sina ila roho inauma...Je roho ikiuma sio ndio wivu???

Tuesday, June 25, 2013

MATESO KATIKA NDOA/MAHUSIANO....KUFUJWA KWENYE NDOA NI NINI?



Ifuatayo ni habari ya mwanamke ambaye aliwahi kuja kwangu kwa ushauri kuhusu ndoa yeke: Mama Kotilda Mkatah aliolewa mwaka 1980 na mume msomi aliyekuwa na wadhifa mkubwa kwenye taasisi moja ya fedha ya serikali.
Ndoa hii ilifungwa kwa sababu, Kotlida hakuwa na njia, lakini anasema, tangu wakiwa kwenye uchumba, alikuwa tayari na wasiwasi kama ndoa yao ingekuwa ni ya amani. Anasema, wakati bado wachumba, huyo bwana aliwahi kumpiga kibao kwenye kituo cha UDA kwa kosa la kuchelewa kufika kituoni kama walivyokuwa wamekubaliana.
Ndoa ilikuwa ni ya mateso makubwa hata kabla haijafungwa, Mwezi mmoja baada ya ndoa, mume alimwachia mkewe kazi kwa kwenda kufanya fujo ofisini kwa bosi wake kwa madai kuwa bosi huyo alikuwa na uhusiano na mkewe. Kotilda alianza kuishi kwa masharti. Hakuna kutoka, hata kwenda kwa jirani bila kuomba ruhusu na kutoa maelezo marefu kwa nini aende huko.
Kusimangwa, kukosolewa, kuitwa mjinga na mbumbumbu, ikaanza kuwa ni sehemu ya maisha ya mama huyu. Hali iliendelea hivi na kotilda akawa anajiambia, kuna siku hali itabadilika. Lakini, kwa bahati mbaya, hali haikubadilika. Wakati anakuja kwangu, alikuwa ameshaanza kuamini kwamba ni kweli alikuwa anastahili kutendewa vile na mumewe.
Huku ndiko tunakoita kufujwa. Mpenzi mmoja anapomuumiza mwingine kwa kauli zake au kimwili, mara kwa mara, tunasema hapo kuna kufujana.
Mpenzi mmoja anapokuwa na mamlaka aliyojipa dhidi ya uhuru na haki ya mwenzake, tunasema hapoimekuwa kufujana. mara nyingi, wanaofuja ni wanaume. Miongoni mwa matatizo ya ndoa ambayo mtu hashauriwi kuendelea kuyavumilia ni kufujwa. Ndoa ya kufujwa kuna maumivu makubwa ya hisia na mwili.
Ni vizuri hata hivyo, nikasema kwamba, neno kufuja ni mimi ambaye nimelibuni keelezea hali hii, ambapo mtu mwingine angeweza kuita mateso katika ndoa, kuonewa katika ndoa au kutumia istilahi yoyote.
Nimeipenda habari hii nikaona si mbaya nanyi wenzangu msome kwani tusinyimane elimu.
Chanzo: kitabu cha Mapenzi kuchipua na kunyauka na marehemu Munga Tehenan.

Monday, June 24, 2013

NIMERUDI KUJA KUANGALIA BUSTANI YANGU MARA MOJA...HIVI NDIVYO BUSTANI ILIVYO BAADA YA MWEZI MMOJA...MTOTO WA MKULIMA NI MKULIMA!!

 HAPA NI MBOGA YA MABOGA ..TENA ILE YA NJOMBE(NYAMUZA) AU PITIKI/SUKUMA WIKI..IMEKUWA HIVI BAADA YA MWEZI MMOJA
 NYANYA ZIMEANZA KUTOA MAUA
 SALLADI AINA YA RUCCULA
 STRAWBERRY/STROBERI
 AINA YA VIUNGO/ÖRTKRYDDOR
 VIAZI MVIRINGO
 VITUNGUU
 FIGIRI
Na hapa ni matokeo ya mboga ya maboga mnayaona mchuma wa kwanza. Kwa hiyo leo ni chakula kila nikipendacho ugali, mboga na maharaga hivi hapa maharage yapo jikoni. Mchicha bado kidogo haujakua ..nitawaonyesha ukikua...Si mnakumbuka hapa....... KARIBUNI TUJUMUIKE KATIKA MLO HUU WA MIKONO YA KAPULYA WENU:-)JUMATATU NJEMA SANA KWA WOTE

Sunday, June 23, 2013

NIPO NANYI KIAINA..NITARUDI KARIBUNI

 Ni hapa ninapumzika ni sehemu nzuri sana kupumzisha akili pia kuwa na familia. Hapa no summerhouse. Nitarudi karibini kuliko mdhaniavyo....panapo majaliwa jioni njema.
 
Na kizuri zaidi sikuhitaji kufunga safari kwenda beach ni dakika mbili tu...

Thursday, June 20, 2013

MDADA KAONA KUWA MODE KWA SIKU MOJA SI MBAYA..AU SIJUI NIBADILI KAZI:-)

 Hapa sijui ndo madoido/madolido au sijui alikuwa anapigana kareti mweee kaaazi kweli
 Na hapa bonge la poozi na miondoka mwanana..hapa ni Jangwani seabreeze resort Dar es salaam. Ni sehemu nzuri sana kupunga upepo..ilikuwa mwaka huu mwezi wa mbili.
 Mmmmh...hizi nywele za kimasai zinawasha ..maana ndo nilikuwa nimesuka tu hapa:-)
Na hapa sijui anasoma misa maana utafikiri anasema bwana awe nanyiii...ni Jangwani tena ...Jioni njema. Na kwa taarifa fupi ni kwamba mkiona nipo kimya msiwe na shaka nipo lakini nitakuwa likizo na ndiyo muda wa kupumzika na kuwa na familia..TUSITUPANE NDUGU ZANGU.. TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA...Kapulya

NIMEJITAHIDI KUIWEKA MAISHA NA MAFANIKIO KAMA MWANZO...

Ama kweli sijui ni nini kimetokea nimeanza kuwiweka tena kama zamani ila sijui kama itakuwa tena kama mwanzo...nasikitika kwa kilichotokea. Pamoja Daima!!!

TAARIFA:- JANA JIONI NIMESHTUSHWA SANA NA MWONEKANO HUU WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO!!

Habari zenu ndugu zangu!
Jana jioni nilijikuta nashangaa au zaidi kama nimepotea pale nilipotembelea blog ya Maisha na Mafanikio. Nini kimetokea sijui kwa kweli ..Je kuna anayejua?...Natumaini ile rangi ya pink itarudi nawaomba kuwa na subira. Na endapo haitarudi basi nitafanya utafiti ni nini kimetokea na nitarekebisha.
Kama kunaanayejua nini kimetokea TAFADHALI tupeane habari.
NAWATAKIENI WOTE SIKU NJEMA.

Tuesday, June 18, 2013

NIMEFANYA UTAFITI KATIKA MILA NA DESTURI ZA WANGONI UPANDE WA NDOA NA KUCHUMBIA/KUOA MKE KUZAA...MTOTO WA KIUME NA KIKE!!!!

Kugega mdala= Kuoa mke
Kama wote tujuavyo:- Kijana na msichana wakikua, wanaoa. Kwa wangoni, mtoto wa kuime hata kama akikua na kuoa atakuwa bado anahitajika kwenda vitani. Kipindi hicho yupo vitani inabidi aonyeshe nguvu zake zote. Kijana ambaye hajaenda vitani huitwa "lijaha". Kijana aliyerudi toka vitani huitwa "lidoda". Mwanamkewa kuolewa inabidi awe wa uhakika, anayeweza  kufanya kazi za nyumbani. Inabidi aweze kutafuta kuni, kuchota maji, kutwanga  kupika ugali/chakula, kupika pombe na awe mchangamfu/mcheshi achekaye na watu wote mtaani/kijijini.
Ndoa haifungwi ndani ya ukoo. Kwa wangoni hairuhusiwi ni mwiko kuoa/kuolewa na mke/mume ambaye ana jina moja la ukoo. kama watu wakioana kiukoo, wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali? (vitepulana) wataapishwa. Watu wanaogopa kuoana ndani ya ukoo kwa vile watoto watakaozaa watakufa wote au watapata kifafa au hata waliokufa (mahoka) watakasirika. Watu wenye Kifafa na wenye ukoma ni mwiko  kuoana.
MTENGA
Kwa kingoni cha zamani neno mtenga lilifahamika kama mtu aanyenunua au kuuza vitu. Pia Mtenga ni mtu auzaye mtoto wa kike. Yeye ndiye anayetoa mahali ya mwanzo na mahali yote kwa ukoo wa msichana.
VIPI KUTAFUTA MKE:-
Wenye mtoto wa kiume watakapo kumwoza kijana wao, wazazi wengine wanamtafutia mke, Wazazi wengine wanamwacha kijana wao ajitafutie mke ampendaye. Kama wame/watamwona msichana mzuri watatafuta mtu/ndugu ambaye watamtaka na watamwelekeza nini wanataka. Na huyo anaweza akawa MTENGA wao. Mtenga huyo ataanza kuulizia kisirisiri mambo ya wazazi wa msichana yule na ukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa mtoto wa kuime. kama wazzi wakiona ya kuwa ni msichan huyu atamfaa kijana wao kama mke ,watenga wataenda kwa wazazi wa msichana tena na kutoa taarifa ya posa. Kama wenye binti watakataa, watenga/mtenga itabidi awabembeleze.....Itaendelea

Monday, June 17, 2013

LEO TUANZE JUMATATU NA KUANGALIA SHULE HIZI ZA KATA YA WINO TARAFA YA MADABA WILAYANI SONGEA!!!

Ifinga ni kijiji ambacho kipo kata ya Wino kutoka barabara kubwa kama inavyoonyesha kwenye kibao ni km 48. Kijiji hiki kinajulikana sana kwa kilimo cha mpunga na machungwa...Mwaka 1992 tulifanya safari mpaka Ifinga tulichukua chumvi nasi tulipata machungwa mengi sana . Kijiji hiki wanakula sana wali hakuna ugali. Ninachoshangaa mwaka ule kulikuwa hakuna hata shule sasa leo napita hapa naona kibao Ifinga Matumbi Secondary school..nikaona ni lazima nipige picha..najiuliza sijui ni maendeleo au ili mradi kila kijiji kiwe na shule?
Kwa sababu mwanzo kulikuwa na shule yetu hii  Wilima ndiyo ilikuwa ya kata. Lakini nayo sasa imeendelea na kuwa High school. Nakumbuka mengi sana kuhusu shule hii....Wilima Sekondari. Kuna nyingi kumbukumbu zinazowahusu watu wengi...Jumatata njema....

Sunday, June 16, 2013

UJUMBE WA JUMAPILI HII YA LEO NI HUU!!!!


Unapotafakari mema ya Mungu ya leo:-
WASAMEHE WALIOKUKOSEA,
WAKUMBUKE WALIOKUSAHAU na UILINDE AMANI YA MOYO ISIPOTEE.
Kwani utakuwa na furaha daima!!!

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA MWENYEZI MUNGU AWE NANYI!!!

Saturday, June 15, 2013

JUMAMOSI YA LEO TUTEMBELEE MJI WA IRINGA..NA WIMBO HUU...

JUMAMOSI IWE NJEMA KWENU WOTE...UJUMBE:- Tumaini huzaa Furaha, Furaha huzaa Amani

Friday, June 14, 2013

UJUMBE WA IJUMAA YA LEO:- NYUSO ZA MWANAMKE!!!

Unajua ya kwamba:- Mwanamke kama dutu la udongo wa mfinyanzi huumbwa na kuumbuliwa na jamii kwa namna mbalimbali. Kama kinyonga, uso wake unabeba rangi tofauti kulingana na mikondo ya maisha na mapigo ya wakati. Itakuwaje mwanamke awe wa kuozwa kama mwenye ugaga wa hisia za kujichagulia mwenyewe; au awe wa kuuzwa kama pakacha la maembe katika soko la umma? Uso wa mwanamke ni njia mbilimbili; ikiwa hazai analea, asipokuwa akirimbesha anarembeshwa, kama hatumbuizwa, ikiwa hajengi anabomoa; na kila mtu anamtazama na kumtarajia aonyeshe  uongofu wa malaika kama kwamba yeye si mtu. Haya yanapokolea ndipo mwanamke anaonyesha nyuso zake.....NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA..KAPULYA

Thursday, June 13, 2013

WATOTO NAO WANAWEZE WAKIPEWA MASOMA....KAZI ZA MIKONO YA WANETU!!!

 NI KAZI YA DADA CAMILLA 2013
 hapa pia ni kazi ya mikono ya dada/binti Camilla mwaka 2012
 na siyo Dada/Binti Camilla tu hata Kaka/kijana Erik naye anaweza ni kazi ya mikono yake mwaka jana 2012
..Na mwaka huu 2013 tena jana amekuja na hii..Hakika kama mama mzazi nimefurahi sana kwa jinsi mikono yao ilivyofanya kazi nzuri. Sina haja ya kununu mito ya mapambo wanangu wananisaidia...Nina haki ya kusema naona FAHARI sana kwa kweli......proud/stolt. ALHAMIS NJEMA KWA WOTE:-)

Tuesday, June 11, 2013

HILI NI CHAGUA LA MAISHA NA MAFANIKIO:- WAREMBO WA WIKI NI HAWA!!!

Hili ni chagua la maisha na mafanikio ...nimependa vazi hili la asili..ni utamaduni na pia wanapendeza ebu angalia na useme lako....JUMANNE IWE NJEMA KWA WOTE....KAPULYA

Monday, June 10, 2013

JUMATATU YA LEO:-KAMA WOTE TUJUAVYO TANZANIA INA MAKABILA 129 NA KILA KABILA INA LUGHA YAKE NAMI LEO NIMEFANYA UTAFITI/MBINU YA NENO AHSANTE SANA...

NENO AHSANTE SANA...TUANZA NA LUGHA YANGU,,,,
Kingoni -  Ahsante sana .......Usengwili sana
Kibena
Kihehe
Kipangwa wao husema ---- Udalike/Tuhongise
Kiha -----------Ulakoze
Kisukuma/ Kinyamwezi------Wabeja kulumba
Kichagga---------Aika mnu
Kinyakyusa------------------------Ndaga fijo
Kinyiramba------------------------Songela
Kifipa-------------------------------Sante kalesa
Kinyambo--------------------------Wakora muno
Kigogo------------------------------Sante muno muno
Msaada zaidi kama kuna anayejua/fahamu lugha nyingine nitashukuru sana..sana...Karibuni....


Sunday, June 9, 2013

NI DOMINIKA/JUMAPILI YA 10 YA MWAKA C...NA TUANGALIE/TUSOME HESHIMA YA MWANAMKE NA WITO WAKE!!!

"Mwanamke kama Mama na mlezi wa kwanza wa mwanadamu ana haki ya pekee kabla ya mwanamume. Umama kwa upande wa utu na maadili unaonyesha uwezo wa mwanamke wa kuumba ulivyo muhimu sana ambao unadhihirisha wito wa pekee na ni changamoto ya pekee inayomchochea mwanamume na ubaba wake"
"Heshima ya mwanamke hutegemea utaratibu wa upendo, nao ni hasa utaratibu wa haki na wa kupendana..."
"Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!" Yesu akajibi, "Barabara; lakini heru yake zaidi yule aliyelisikia neno la Mungu na kulishika"

Saturday, June 8, 2013

KILIMANJARO IONEKANAVYO TOKA ANGANI PICHA KAKA ERIK 2013 JANUARI

 mlima wetu Kilimanjaro
Hakika unapendeza na tuna haki ya kuutangaza mlima wetu Kilimanjaro...
nawatakieni wote JUMAMOSI NJEMA. UJUMBE WA LEO:- Vitu muhimu katika maisha sio vitu.

Friday, June 7, 2013

KAPULYA ANAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA!!!


IJUMAA NJEMA KWA WOTE!!!

MWONEKANO MPYA WA BLOG YA KAKA MFALME MROPE!!!

Ndug zangu habari za leo!
Nadhani wote mu-wazima wa afya njema. Dhumuni langu leo ni kutaka kuwapa habari au kuwaambia ya kwamba blog ya http://tustaarabike.blogspot.se/ imebadili muonekano na imehamia au inaitwa sasa http://jehuuniuungwana.com/....na mmiliki ni yuleyule kaka Mrope.
Nawatakieni kila la kheri na kila jambo mtakalofanya..Ijumaa yenu iwe yenye amani. Kapulya:-)

Thursday, June 6, 2013

BLOG MPYA KUANZISHWA...KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA KUBLOG...

Ni blog  mpya iliyoanzishwa hivi karibuni kwa kutaka kujua zaidi ni nini inaibui tembelea hapa... karibu sana ndugu yetu.

LEO TUBURUDIKE NA KIODA KUTOKA KWETU LIULI KARIBUNI!!!


Liuli ni moja ya vijiji ambacho kipo kando ya ziwa Nyasa ni maarufu kwa hospitali na jiwe hili hapa chini ...pia kahitoria kidogo juu ya hili jiwe na mji wa Liuli..

Jiwe la Pomonda

Miongoni mwa miji muhimu katika wilaya ya Nyasa ni mji wa Liuli. Mji huu unayo bandari muhimu ambayo hutumiwa na meli zinazofanya safari katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. meli za Mv Iringa na Mv Songea zimekuwa zikitia nanga katika bandari hiyo ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi, usafirishaji bidhaa na kadhalika.
Katika rekodi za kihistoria kuna mengi ya kukumbukwa katika mji wa Liuli, lakini jambo muhimu ni kuwepo kwa Jiwe hilo ambalo linalinganishwa na sura ya binadamu. Ukkchunguza jiwe hilo utaona linafanana kidogo au kuwa na maumbile fulani yenye sura ya binadamu.
Ni historia nzuri na tamu kwa wakazi wa nyasa na vitongoji vyake. Jiwe hilo lipo karibu kabisa na Bandari ya Liuli ambapo kila abiria au msafiri yeyote anapotumia bandari hiyo ataweza kuliona. Ni moja ya vivutio vya Utalii katika mji wa Liuli. KARIBUNI WATALII, KARIBUNI LIULI kujionea mengineyo.

Tuesday, June 4, 2013

MILA NA DESTURI:- NI WAZO LA LEO KUTOKA KWA DIARY YANGU....EBU SOMA HAPA CHINI!!!

Katika pitapita zangu kila siku nakutana na mengi sana katika blog nyingi na hivi karibuni nilikuwa nimepita hapa na nikakutana na WAZO la mwanablog mwenzetu nimelipenda wazo lake nami nikaona si mbaya kama nikaleweka hapa ili kueneza wazo lake.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WAZO LA LEO: Mila na desturi zipo, na tumezikuta kwa wazee wetu, zipo nyingi, na nyingi hatuzijui tena kwa vile huenda hazikuwezekana kutekelezeka. Lakini kuna mambo mengi mazuri tumeyapuuzia, na kwa kufanya hivyo tumejikuta tukipata taabu sana,…nachukia kwa mfano wa kutafuta mchumba, kabla mtu hajaoa au kuolewa, wazee wetu walikuwa wakihakikisha kuwa mke au mume wa kuoa au kuolewa anatafutwa kwa kufanyika uchunguzi wa kina kwenye familia anayotoka…ni ni hekima yake, ni kuwa kwa kumpata mume au mke bora ni kwa ajili ya kizai bora, na matokeo yake ni kuwa na familia bora na hili litaweza kujenga taifa lenye amani, hili tumelipuuza, na matokea yake ndio haya..
Pia wazee wetu walikuwa wakiangalia kuwa huyo anayeolewa au kuoa, hana matatizo yoyote ya kiafya au ya kurithi, au tabia za kishirikina, au tabia zozote mbaya…haya yalikuwepo na ukiyachunguza kwa makini utayaona kuwa yalikuwa na faida zake, lakini huenda haya na mengine mengi hayapo tena tumeyapuuza.
Wazo langu la leo. Zipo mila nzuri, tuzifuate, na kama zipo mila potofu, tuziache, au tuziboreshe ziwe bora zaidi, lakini tusisahau kabisa mila na desturi zetu zenye hekima ndani, na kukimbilia mila na desturi za wenzetu,….kwanini tupuuze mila zetu, ….huo ndio utamaduni wetu na anayeacha utamduni wake ni mtumwa.
NIWATAKIENI JUMANNE NJEMA NA KILA MTAKALOTENDA LIWE NJEMA...UJUMBE TUPENDANE....KAPULYA WENU

Monday, June 3, 2013

JUMATATU YA LEO TUANZA NA KUMPA HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ERIK!!!!

Twapenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kumjalia kijana Erik afya njema. Na leo hii tarehe hii ndio ametimiza miaka 13...HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KIJANA ERIK...Na twakutakia mafanikio mema kwa yote unayotarajia kufanya.





Saturday, June 1, 2013

MWEZI MPYA NIMEANZA HIVI:- NIMEFURAHI SANA KUUPATA WIMBO HUUU ..EBU SIKILIZA NA UNGANA NAMI KUCHEZA ..EEEHHHH CHEKETU

HUU NI WIMBO WA ASILI AMBAO NI WA WENYEJI WA MKOA WA RUVUMA NCHINI TANZANIA. WIMBO HUU UNAPATIKANA KWENYE ALBAM MWANA WA SHULI SHULI, MAANA YAKE MTOTO WA SHULE. WOTE MUWE NA JUMAMOSI NJEMA MIE HAPA NIPO HOI KABISA..KACHIKI NA WENGINE HAYA TWENDEEE twende mpaka asubuhi.....